Deuteronomy 12:5-10

5 aBali mtatafuta mahali Bwana Mwenyezi Mungu wenu atakapopachagua katika makabila yenu yote ili aliweke jina lake huko kuwa makao yake. Mahali hapo ndipo iwapasapo kwenda; 6 bhapo ndipo mtakapoleta sadaka zenu za kuteketezwa na dhabihu, zaka zenu na changizo zenu, kile ulichoweka nadhiri kutoa, sadaka zenu za hiari na malimbuko ya makundi yenu ya ng’ombe pamoja na mbuzi na kondoo. 7 cHapo, katika uwepo wa Bwana Mwenyezi Mungu wenu, ninyi pamoja na jamaa zenu, mtakula na kufurahia kila kitu ambacho mmegusa kwa mikono yenu, kwa sababu Bwana Mwenyezi Mungu wenu amewabariki.

8 dMsifanye kama tunavyofanya hapa leo, kila mtu anavyopenda mwenyewe, 9 ekwa kuwa bado hamjafikia mahali pa mapumziko na urithi ambao Bwana Mwenyezi Mungu wenu anawapa. 10 fLakini mtavuka Yordani na kuishi katika nchi Bwana Mwenyezi Mungu wenu anayowapa kama urithi, naye atawapa pumziko kutokana na adui zenu wote wanaowazunguka ili ninyi mpate kuishi kwa salama.
Copyright information for SwhKC